Usijisikie vibaya kuona watu wa karibu au wa mbali hawaelewi wala hawapo tayari kukuelewa kuhusu mapambano yako. Inaumiza kuona watu ambao unawapenda na kuamini inaweza kuwa wazazi, ndugu, jamaa, rafiki au wafanya kazi wenzako. Kuna nyakati unaweza ukawa unafanya kitu lakini hakuna anaeunga mkono jitihada zako ata ukiwaeleza wanakugeuzia shingo. Sasa Nini Ufanye Pale Unapitia Hali Ya Kutoeleweka Kwenye Mapambano Au Utafutaji Wako?
- Kubaliana na hali iliyopo. Wengi huwa wanapenda kuonekana miongoni mwa watu wengi ata kama wanachokifanya kinathamani kuliko hao watu wengi. Ukiona umekataliwa usirudi nyuma, endelea kusonga mbele adi pale watakapokuona kuwa mfano. Jambo la msingi ni kua anayelijua tumbo lako ni wewe na mwili wako, shida zako wengine ni furaha zao.
- Tafuta sehemu yenye uhuru na utulivu. Ondoka sehemu usiokubalika nenda sehemu ambayo utapat utulivu wa akili, sehemu ambayo unaweza kufanya kazi zako kwa uhuru bila ku na msongo wa Mawazo. Unaweza ukasafiri kutoka mkoa uliopo au nchi uliopo Kwenda sehemu nyingine. Hii itakusaidia kujifunza mazingira mapya na kupata watu wapya. Mtu asiekufahamu hutoa thamani kubwa kwenye kile unachokifanya kuliko ndugu wako wa karibu.
- Usioneshe hasira endapo unakataliwa. Kila unachokifanya hakikisha hasira yako haidhihiriki mbele ya adui zako. Siku utakapoonesha kuchukizwa na jambo fukani ndiyo siku utakayomruhusu adui kukudhuru zaidi. Udhaifu wako ni silaha dhidi yako, kamwe usijeonesha udhaifu wako kwa adui yako.
- Punguza kuweka mambo yako hadharani. Ukifikia hali hii acha kuwaambia kila kitu acha waone jambo limekwisha tendeka. Uchunge ndimi zako kwa hali na mali. Si kila mtu anashindwa kukuelewa wakati wa mapambano yako bali wengine wanafanya hivo ili uwaelezee zaidi waweze kubeba mbinu zako, hivyo punguza kujieleza.
- Endelea kujenga imani yako. Katika hali kama hii weka imani yako kwenye matokeo unayoyaamini na achana kabisa na imani za watu wanaokuvunja. Hizi ndio nyakati ambazo vitu vingi muhimu hupotea. Utapoyumbishwa kidogo ukakubali kuyumba ata mipango yako hufifia. Kikumbwa mtangulize Mungu wako kisha amini kile unafanya na kifanye kwa juhudi.
Hakuna kitu kimewekwa kutukwamisha ila sisi wenyewe. Ni lazima tujue nini kinahitajika na kwa wakati gani. Tutengeneze desturi za kutuongoza katika nyakati ngumu na nyepesi. Nipo hapa kukuandalia nakara mbalimbali za kukusaidia katika Nyanja tofauti ikiwemo teknolojia, afya, Uchumi, maisha halisi na kukuletea historia mbalimbali hivo jiandikishe kwenye jarada langu ili usikose nakala inayofata. Kama umependa nachokifanya unaweza onesha upendo wako hapa. Wasiliana nasi moja kwa moja hapa.